Kubadilisha ADA hadi Shilingi za Kenya kwa kutumia Yellow Card
Ili kubadilisha ADA yako kuwa shillingi za Kenya, unahitaji kuwa na vitu hivi 3:
- Pochi la Cardano
- Akaunti ya Yellow Card
- Nambari inayotumika ya Mpesa
Hatua za kubadilisha ADA kwa shilingi za Kenya
Tutachukulia kuwa tayari una pochi la Cardano, na nambari inayotumika ya Mpesa. (Ikiwa unahitaji pochi la Cardano, angalia maagizo hapa)
Kitu cha mwisho unachohitaji ni akaunti ya Yellow Card. Hapa kuna hatua za kuunda akaunti:
- Nenda kwa Yellowcard.io
- Bofya kwenye "jisajili" ili kuunda akaunti
- Jaza maelezo yanayohitajika. Kumbuka kutumia majina yaliyopo kwenye kitambulisho (Kitambulisho cha Taifa) na kuongeza namba ya simu ambayo imesajiliwa kwa huduma za Mpesa.
- Thibitisha nambari yako ya simu na anwani yako ya barua…