Project Catalyst- Taswira ya Africa

Lido Nation inakutana na watu wenye taswira jijini Nairobi

Wiki iliyopita tulianza safari iliyohamasishwa na blockchain huko Nairobi, Kenya. Katika makala ya wiki iliyopita, nilielezea nilichojifunza kutokana na utafiti na uzoefu wangu wa kibinafsi katika bara hilo kuhusu kwa nini Afrika ni muhimu kwa zana za blockchain Pia nilitambulisha miradi ambayo Lido Nation tayari imezindua jijini Nairobi - yaani Ngong Road Blockchain Lab.

Wiki hii tunaelekeza macho yetu kwa siku zijazo. Nikiwa Nairobi, nilishangazwa na fursa na mazungumzo yaliyojitokeza ndani ya siku 10 fupi nilizokua uko. Kulikuwa na hamu na shauku kubwa ya kujifunza, kujaribu kitu kipya, na kufanya kazi pamoja kwa maisha bora ya baadaye.

Swahili Learn-to-Earn

Katika Hazina maalum ya 9 ya project catalyst, Lido Nation ilifadhiliwa ili kuendeleza kazi yetu katika mataifa yanayozungumza kiswahili Afrika kwa mradi wa “swahili learn to earn”. Ilikuwa ni sadfa kubwa kwamba nilikuwa Nairobi katika maabara ya Ngong Road Blockchain nilipopata barua pepe yenye matokeo ya kura ya Fund 9 na kugundua tulikuwa tumeshinda ufadhili wa mradi huu. Laiti kila mtu aliyetupigia kura angeshuhudia msisimko kwenye Maabara! Asante kwa kura zako, na usiwe na shaka Project Catalyst inabadilisha maisha.

Ngong-Road-Lab

Kwa kutumia nyenzo za elimu za Lido Nation ambazo tayari zimetafsiriwa kwa Kiswahili, tunaunda zana ya kujifunzia yenye motisha, na hivyo kupanua ufikiaji wa nyenzo hizi. Wazungumzaji wa Kiswahili wanaweza kushiriki kwa kufungua pochi la Cardano,na kuunganisha kwa Lido Nation, kusoma makala, kujibu maswali kwa Kiswahili, na kupokea kiasi kidogo cha ada kama zawadi yao ya ushiriki. Kupitia mradi huu, tunatarajia kuundwa kwa mamia ya pochi mpya za Cardano barani Afrika, kila moja ikiwa na ada kidogo. Kwa Haya yote, ufahamu wa washiriki utakuzwa na maarifa mapya kuhusu ugatuaji wa blockchain, Cardano, na project catalyst.

Jinsi unavyoweza kushiriki: Ikiwa una uhusiano na watu, mashirika, au jamii katika Afrika wanaozungumza Kiswahili, waambie kuhusu Lido Nation. Tayari tuna zaidi ya makala 40 zinazopatikana katika Kiswahili. Kuanzia mwaka wa 2023, watumiaji wanaozungumza Kiswahili wataweza kupata ada kwenye tovuti kwa kusoma makala na kujibu maswali kuhusu maudhui.

DirectEd.Dev

Mradi huu wa project catalyst mradi ulivutia macho yangu kama Mtathmini wa Pendekezo ( Proposal Assessor) katika hazina maalum wa 8, na pendekezo lao la kujenga “Jukwaa la udhaminia/mchango kulingana na Atala PRISM inayowezesha michango salama, ya gharama ya chini, yenye masharti ya rika-kwa-rika kwa wanafunzi.” Hii ilikuwa sawa na historia yangu katika elimu na mashirika yasiyo ya faida. Nia yangu iliongezeka nilipojifunza kwamba walilenga shule ya upili jijini Nairobi kwa majaribio yao ya mradi. Nikiwa Nairobi, timu ya maabara ya blockchain na mimi tulipata bahati ya kukutana na kiongozi Nairobi wa mradi huu DirectEd, Moses.

DirectEd-Lido-Nation

Wawakilishi kutoka Lido Nation, DirectEd, na Ngong Road Blockchain Lab - mkutano wa mawazo

Kulingana na makala ya Forbes.com , tunakabiliwa na upungufu wa wasanidi programu unaofikia mamilioni ndani ya miaka mitatu ijayo; wengi tayari wanahisi athari za suala hili linalokua leo. DirectEd inashughulikia suala hili moja kwa moja kwa kuelekeza rasilimali za mafunzo na ufadhili wa masomo ili kukuza ufanyakazi ya wasanidi wa Kiafrika. Nilijifunza kwamba wanafafanua lengo la mpango wao wa ufadhili wa masomo, kulenga wanafunzi wanaopenda ukuzaji wa kompyuta, na kutoa nyenzo zinazolengwa za mafunzo ya wasanidi ili kuimarisha athari za programu.

Jinsi unavyoweza kushiriki: Unaweza kusikiliza mahojiano mazuri na mwanzilishi wa DirectEd Simon Sallstrom, angalia ripoti za kila mwezi za mradi kwenye tovuti yao, na uzifuate kwenye Twitter.

Safi.Eco

Kupitia miunganisho ya mtandao, nilifurahia kukutana na Joe kutoka kwa mradi wa nascent blockchain safi.eco . Mradi huu ni mpya sana hivi kwamba bado hawajaamua ni blockchain gani watashirikiana nazo. Walakini, wana maono mazuri ya jinsi blockchain inaweza kuwezesha uvumbuzi wa kupendeza wa siku zijazo. Safi ina maana isiyochafu katika Kiarabu na Kiswahili. Kutoka kwa timu yao, nilijifunza kwamba nchi nyingi za Kiafrika kama Kenya zimeongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wao wa uzalishaji wa ndani katika miaka za hivi majuzi, ambayo imesababisha ongezeko la uwiano wa mahitaji ya nishati. Hata hivyo, taratibu za ufadhili za polepole na zisizo na tija zimezuia utumaji wa rasilimali mpya za nishati. Inaweza kuchukua watumiaji, kama vile wakulima, miaka kadhaa, na kwa viwango vya juu sana vya riba, kununua vifaa vya kuzalisha nishati kama vile paneli za jua

Safi-Eco

Itifaki ya Safi inaziba pengo hili la soko kwa kutumia uwezo wa Web3 kuunganisha ufadhili wa hali ya hewa duniani kwa miradi ya nishati ya ulimwengu halisi kwa kiwango kisichocha juu. Wanarudisha umiliki na ukuzaji wa mali za kukabiliana na hali ya hewa hadi mashinani kwa kurahisisha uwekezaji, kununua, kukopa na kulipia nishati mbadala rahisi kama vile kutumia TikTok. Maono yao ni kwamba ili kuharakisha mchakato wa kuondoa kaboni katika uchumi, lazima tufanye kazi pamoja kama jamii ya kimataifa ili kufanya kukabiliana na hali ya hewa kuwa rahisi, kufanya uwekezaji, haraka na kwa uwazi.

Safi-Eco-2

Jinsi unavyoweza kushiriki: soma zaidi kuhusu mradi na ujiandikishe iliupate sasisho kwenye tovuti yao, Safi.Eco. Ikiwa una mradi au wazo la nishati safi na ungependa kuungana na timu ya Safi.Eco, tuma barua pepe kwa: [email protected]

Smart Farming - Ubunifu wa Kijeshi katika Maonyesho ya Biashara ya Nairobi

Kichwa hiki cha mwisho kiko mbali kidogo na njia ya blockchain, lakini kwangu, kilijumuisha kile nilichoona Nairobi kuhusu uwezo ghafi katika eneo hili. Nilibahatika kuhudhuria “Maonyesho ya Biashara” ya kila mwaka ya Nairobi – tukio la kufurahisha na la kuelimisha ambalo huleta wingi wa mabasi ya watoto wa shule kutoka pande zote.

Nairobi-Trade-Fair-pig-barn

Hapa niko kwenye Banda la Nguruwe kwenye Maonyesho ya Nairobi

Maonyesho hayo yalifanana sana na maonyesho ya jimbo langu (Marekani ya Kati Magharibi), pamoja na maonyesho ya kilimo, majengo ya elimu, vibanda kutoka kwa tasnia nyingi, na bila shaka, vyakula vingi vizuri vya mitaani.

Nairobi-trade-fair-juice-stand

Chakula Kizuri chenye ladha ya Kiafrika: miwa, tangawizi na ndimu zilizokamuliwa / kusagwa ili kuagizwa!

Kibanda kimoja katika maonyesho makubwa ya kijeshi ya Kenya kilionyesha ubunifu mpya wa kilimo kwa wakulima wa Kenya. Ninatoka katika familia ya wakulima, kwa hivyo ninafahamu baadhi ya uvumbuzi katika kilimo cha Marekani, ikiwa ni pamoja na matrekta makubwa kuliko nyumba, yanayoendeshwa na roboti za GPS. Kinyume chake, zana mpya za kilimo ambazo “zinaboreka” nchini Kenya ni za ukubwa wa binadamu, zinazotumia nishati ya jua, au tu kutumia kitu kama gia za baiskeli ili kufanya maisha kuwa rahisi na yenye tija zaidi kwa mkulima mdogo.

military-farm-innovations-Nairobi-Kenya

Mashine ya kupandia kwa kutumia nishati ya jua na binadamu, kinyunyizio cha kunyunyizia mazao kwa kutumia shimo nyingi, na kitenganishi cha mafuta kinachotumia nishati ya jua. Kila moja ya hizi hutumia teknolojia inayoweza kufikiwa na endelevu ili kutoa uboreshaji mkubwa kwa kazi zinazofanywa kwa mikono sasa

Nairobi-fair-agriculture-test-plots

viwanja vya majaribio vinavyoonyesha mazao tofauti na mbinu za ukuzaji.

Kutokana na hali hii, bango lilielezea programu mpya kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa inayoitwa “MaziwaSoko“ (Soko la Maziwa). Kwa sasa, wafugaji wengi wa maziwa vijijini hawana uwezo wa kupata taarifa za uwazi kuhusu bei ya maziwa na taarifa nyingine muhimu kwa biashara zao. Kwa matokeo yake, yanaonekana kwa waendeshaji katika soko “isiyo rasmi” ambao hununua maziwa yao kwa bei yoyote ambayo wanaweza kupata. Programu ya MaziwaSoko inaanza kutambulisha uwazi na uwekaji kumbukumbu sokoni kwa wakulima ambao hapo awali hawakuwa na ufikiaji rasmi wa zana hizo. Kwa sisi tunaovutiwa na blockchain, maneno kama vile “uwazi” na “rekodi” za kuaminika ni kama maneno ya ufunguzi wa wimbo wetu tunaopenda. Katika sehemu za ulimwengu unaoendelea kama Nairobi, watu wanavutiwa na teknolojia hii si kwa sababu tu inavutia lakini kwa sababu mahitaji ni mengi sana na yanahitajika sana.

Jinsi unavyoweza kushiriki: Unapofikiria kuhusu mradi wako unaofuata wa blockchain, zingatia kuungana na jamii zinazokua barani Afrika. Jamii ya Cardano tayari ina watu wanaofanya kazi katika bara hili na nia ya wazi ya jamii katika kuongeza ahadi hiyo kupitia project catalyst na ushirikiano mwingine. Miradi mingine ya Cardano ya kuchunguza barani Afrika itajumuisha Empowa na Wada.

Hitimisho

Asante kwa kujiunga nami kwa simulizi hili la onyesho la safari yangu! Ikijumlishwa, miradi na watu niliopatana nao walikuwa na maneno ya kutia moyo,na kuhusu kile kinachosisimua kuhusu blockchain, Cardano, na Project Catalyst. Ikiwa umekuwa ukifwatilia kwa umbali nakuhimiza uje ujiunge nasi..

Kama hatua ya kwanza, sajili pochi yako ili upige kura katika hazina maalum ya 10. Nenda kwenye makala haya mazuri kuhusu kujiandikisha kupiga kura kwenye project catalyst ukiwa tayari kuanza!

Iwapo unahitaji kupata ada 500 ili kuhitimu kupiga kura, pata Mafunzo yetu ya Mkaguzi wa Pendekezo(proposal assessor) bila malipo ili kushiriki katika hazina maalum ya 10 katika jukumu hilo; mtathmini mwenye bidii anakaribia kuhakikishiwa kupata ada kiasi hicho kwa kazi ya siku ya uaminifu kama mtathmini.

Ikiwa una hamu ya kujua aina nyingine za miradi zinazofadhiliwa kupitia project catalyst, tembelea zana yetu ya Catalyst explorer tool, ambapo unaweza kugundua mapendekezo na miradi inayofadhiliwa ya aina zote.

Ikiwa uko tayari kuanza kujenga jamii ya cardano, zingatia kutuma maombi ya ufadhili katika hazina maalum ya 10! Hata kama hutashinda ufadhili kwa mara ya kwanza, una uhakika wa kupokea maoni kutoka kwa jamii na kupata marafiki wapya wanaoshiriki maslahi yako, ambayo itasababisha jambo linalofuata katika safari yako.

Ikiwa una maswali kuhusu mojawapo ya njia hizi za kushiriki, tafuta “Project catalyst “ katika utafutaji wetu wa kimataifa ili kupata makala mahususi muhimu - au wasiliana nasi!

Get more articles like this in your inbox

Was the article useful?

Or leave comment

No comments yet…

close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00