Cardano tayari ina uwepo mkubwa barani Afrika na inapanga kwenda mbali zaidi kutambuliwa katika nchi nyingi zaidi za Kiafrika.
Charles Hoskinson, mwanzilishi wa Cardano, amezungumza juu ya uwezo mkubwa wa bara la Afrika kwa kukubalika na kujulikana kwa teknolojia ya blockchain. Wakati wa mahojiano na John O`Connor, ambaye ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kiafrika katika IOG alitangaza kuwa miradi ya IOG barani Afrika ni nzuri.
IOG kwa sasa inashirikisha wenyeji kwa kutoa miradi inayosuluhisha matatizo ya ulimwengu halisi. Kumekuwa na kampeni ya mara kwa mara ya ufadhili katika project catalyst “Grow Cardano Grow Africa” ambayo inaangazia Afrika. . Kupitia miradi hii, Afrika inapata usaidizi, miradi ya kibiashara inayojengwa barani Afrika inapata usaidizi kutoka kwa jamii, na Cardano inapata kukubalika na watu wengi. Hapa kuna baadhi ya mifano ya nchi za Kiafrika ambazo zinafanya kazi na Cardano;
Cardano nchini Ethiopia
Serikali ya Ethiopia inafanya kazi na Cardano kuwanufaisha wanafunzi milioni tano. John O`Connor , mkurugenzi wa uendeshaji wa IOHK wa Afrika alisema, “Mabadiliko ya elimu ya blockchain ya Ethiopia ni hatua muhimu katika dhamira ya IOHK ya kutoa vitambulisho vya kiuchumi na ajira, huduma za kijamii na kifedha kwa waliotengwa kidijitali,”
Ethiopia itatekeleza kitambulisho cha kitaifa cha blockchain, cha mwanafunzi na mwalimu na mfumo wa kurekodi mafanikio ili kuthibitisha alama, kufuatilia utendaji wa wanafunzi ili kuongeza elimu na ajira. Lengo la hili ni kuwapa wanafunzi sifa za kidijitali zilizothibitishwa za blockchain ili kupunguza ukosefu wa uaminifu katika vyuo vikuu na kuongeza uhamaji kwa kuruhusu waajiri kuthibitisha alama zote za waombaji kazi.
Kando na elimu, IOHK iko kwenye majadiliano kuhusu mfumo wa tiketi wa uchukuzi wa kidijitali wa blockchain katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
Cardano nchini Tanzania
Kama ilivyotangazwa awali, Cardano ilipata mkataba wa pili wa ushirikiano na Tanzania unaolenga kujenga miundombinu mibaya nchini humo.
Tanzania ni nchi ya Afrika Mashariki. Tanzania inashirikiana na Cardano kuwezesha kuunganishwa kwa mtandao wa simu, utambulisho wa kidijitali na uwezeshaji wa kifedha kwa jamii za vijijini nchini.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa, kampuni hizo zitaanzisha mradi huu kutoka Zanzibar. Lengo kuu litakuwa kutoa muunganisho bora wa intaneti huku ukitumia vyanzo endelevu vya nishati inayotumia nishati ya jua. Watakuwa wakitoa mtandao wa simu kwa wale ambao hawana. Wanafanya kazi na mtandao wa simu nchini Tanzania unaoitwa Telecom na wanapanga kuwapa watumiaji wake utambulisho wa kidijitali na kuwa na ADA kama njia ya malipo.
Cardano nchini Kenya
Cardano pia iko nchini Kenya kupitia pendekezoambalo Lido Nation lilishinda. Kupitia mradi huu Cardano imeunda maabara ya kwanza ya blockchain nchini Kenya, inayojulikana kama Ngong Road Blockchain Lab iliyoko Nairobi, Kenya. Mradi ulianza mwaka jana na wanafunzi wawili wachanga wa vyuo vikuu ambao ni watengenezaji wa wavuti. Mapema mwaka huu timu iliongeza wanafunzi watatu zaidi ambao wanasimamia utafsiri wa makala kwa Kiswahili. Lengo la hili ni kufanya mataifa mengi yanayozungumza Kiswahili kuweza kujifunza zaidi na kuelewa zaidi kuhusu Cardano na kuipa cardano uwezo wa kujulikana na kukubalika na watu wengi.
Ili kujifunza zaidi kuhusu mradi huu hapa kuna makala juu yao, https://www.lidonation.com/en/posts/announcing-lidonation-launches-cardano-blockchain-lab-in-kenya
Conclusion
Muungano kati ya Afrika na Cardano unalenga kubadilisha nchi zote 54 kuwa soko la kidijitali. Wanataka kuwekeza katika miundombinu ya kidijitali ili kuruhusu viwanda kukua na kutengeneza fursa katika uchumi wa Afrika, hii ni pamoja na uwekezaji katika mtandao, elimu, usafiri na mengine.
Hii ni mifano michache tu ya ushirikiano wa miradi ya Cardano barani Afrika. Miradi hii imefanya Cardano kupata kutambuliwa na kupitishwa kwa wingi barani Afrika. Iwapo utakuwa na mradi/ pendekezo ambalo linaweza kukuza Afrika na kukuza Cardano unaweza kuzituma kwenye https://cardano.ideascale.com/ ili kupata ufadhili.
No comments yet…